KUKABIDHI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Security, Eric Kibet Sambu, akikabidhi moja ya kiti cha wagonjwa kwa Mkurugenzi wa Uuguzi wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI), Flora Kimaro, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo Dar es Salaam, jana, kuitikia maombi ya misaada ya kibinadamu kwa taasisi hiyo kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa ambao hawana ndugu wa kuwasaidia. (Na Mpigapicha Wetu)

Add a comment

KUZINDUA

Balozi wa Kuwait nchini, Jasen Al-Najem na Diwani wa Kata ya Mburahati, Yussuf Yenga (kushoto) wakizindua kisima cha maji safi cha Shule ya Msingi Baridi Mburahati jijini Dar es Salaam jana kilichojengwa chini ya udhamini wa taasisi ya The Holy Qur’an Memorization Charitable Trust. Kulia ni viongozi mbalimbali wa eneo hilo. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

MAZOEZI - YANGA

Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi kwenye Gym ya City Mall, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 26. (Picha na Rahel Pallangyo).

Add a comment

KUIMBA

WAJUMBE wa Mkutano wa 19 wa mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakiimba wimbo wa jumuiya hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Dar es Salaam leo.

Add a comment

KUOKOA

Wananchi wakimuokoa dereva wa lori aina ya Fuso, Amir Mboriko baada ya kunusurika kifo yeye na utingo wake kufuatia lori alilokuwa akiendesha likiwa na shehena ya mchele kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa Mapinduzi, Uyole mkoani Mbeya jana. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment